Habari ndugu mkulima
Ni wakati wa kilimo sasa ni vyema kuandaa shamba mapema ili kuendana na mfumo wa hali ya hewa kwa mvua kuwahi au kuchelewa
Napenda kuwakumbusha kujinga kwenye mfumo wa ruzuku wa segikali ili kuweza kupata mbegu na mbolea kwa bei nzuri yenye punguzo la serikali.
Kilimo cha mahindi ni kilimo mama kwa Tanzania mana ndilo zao letu kuu la chakula. Ni vyema kuendelea kujifunza na kulifanya zao la kibiashara pia ili kujitengenezea kipato zaidi na zaidi kupitia zao hilii
Ili kufikia malengo ni lazima kuwa na mpango kazi wa uzalishaji wenye tija
1.fahamu unataka kulima eneo gani
2.fahamu ukubwa wa eneo unalotarajia kulima zao husika
3.anda bajeti kulingana na ukubwa wa eneo ukijumuisha shuguli zote za uzalishaji utakazofanya uwapo shamanic
4.uwe na nguvukazi ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia mazao shamani
5.andaa mbegu nzuri
6.andaa shamba kwa wakati kabla mvua hazijaanza kunyesha hii itasaidia kupanda kwa wakati mazao yako
7.hakikisha mbolea ya kupandia kukuzia na kubebeshea ipo tayr
Mkulima ukishaanda haya mambo saba muhimu sasa unaweza anzisha kilimo chenye tija cha zao la mahindi
Karibu kwa makala ya pili kuhusu namna ya kupanda zao la mahindi kwa utaalam
Imeandaliwa na
Robin praise kashanga
Mtaalamu wa maswala ya kilimo na ufugaji
Kwa mawasiliano
0617994897,
Email robinpraise5@gmail.com





