Jumanne, 13 Agosti 2019

  KILIMO CHA MIWA SEHEMU YA 2
karibu tena katika sehemu ya pili ya kujifunza makala ya kilimo cha miwa;
 
KUPANDA
   baada ya kuandaa mbegu yako vizuri unatakiwa kuipanda kwa wakati. shamba linatakiwa liwe limeandaliwa vizuri kwa mifereji au mashimi mazuri ili uweze kuufukia vizur usiungue na jua wakati wa jua kali.

NAFASI (SPACING)
    ni vyema kuweka nafasi nzuri kati ya msitari na mstari au shina ana shina la mua ili kuupa nafasi nzuri kuendelea kuzaliana na pia kuweka nafasi nzuri wakati wa palizi uweze kupalilia vizuri bila kuijeruhi mizizi yake. Unashauriwa kuweka nafasi ya mita moja kati ya mstari na mstari wa miwa au cm 75

UMWAGILIAJI
   Miwa inahitaji maji ya kutosha ili iweze kuzaliana vizuri shamban kwako na kuweka maji na sukari ya kutosha. angalizo        pindi unapopanda muwa tu unatakiwa kumwagili kila siku kwa siku 5-7 ili kuwezesha muwa uchipue haraka na vizuri. Ziko njia mbali mbali za umwagiliaji kwa kufungua maji kwenye bwawa na kumwagilia kwa jembe au kumwagilia kwa mashine
   ni vyema kama huna mashine uweki vizuri miundombinu yako ya umwagiliaji ili kuweza kupata urahisi wakati wa kumwagilia.

MBOLEA
   ni vyema kutumia mbole zifuatazo kwa ajili ya kupandia
       1. samadi kama inapatikana kwa wingi itumike kwa kupandia
       2. DAP
       3. SA
 Kwa mbolea za kukuzia ni vyema kutumia kama
    - URE
    - CAN
    - MOP
Pia unaweza kutumia mbolea za kampuni ya YARA KULINGANA NA MAELEKEZO YA MUUZAJI NA KAMPUNI YENYEWE

PALIZI
    ni muhimu kufanya palizi mapema kwenye miwa ili kufanya uzalishaji wa miwa kuwa vizuri na kuzaa kwa wingi pia hupunguza magonjwa kwenye miwa.
unaweza fanya palizi kwa nyia 2
1. kupalilia kwa jembe la mkono
2. kutumia madawa
   Baadhi ya dawa za magugu ni
- Diuron
- Volismer
-Grayphasety (round up)
   kwa matumizi nya dawa hizi tafadhali usitumie bila kupata maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo.

KUKOMA NA KUVUNA
   Miwa huchukua miezi 10 had 13 kukomaa na kuvunwa ni vyema miwa ivunwe mapema kaabla ya kuchanua hivyo kuweza kupata sukari ya kutosha.
   miwa huchomwa kwanza ndio ivunwe ili kupandisha sukari na kupunguza takataka pindi unapopita kwenye mashine wakati wa kutengeneza sukari.

kwa maelezo zaidi karibu  kwa mawasiliano
  0686060797
email; robinpraise5@gmail.com
Robin Praise Kashanga
Dar es salaamu -Kigamboni (kibada)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni