Jumamosi, 11 Mei 2019

MWONGOZO JINSI YA KULIMA MIWA

KIKIMO CHA MIWA







  Miwa ni zao pendwa sana na binadamu wengi sana nchini tanzania, Miwa ni zao linalolimwa kwa ajili ya biashara na matumizi mengine kama tunda.
   nchini tanzania kilimo cha miwa hulimwa kwa baadhi ya mikoa kwa ajili ya biasahara, mikoa inayolima mua ni kama;


  - kilimanjaro
  - kagera
  - morogoro
  - pwani
 sehemu zote hizii hulima miwa kwa ajili ya kuzalisha Sukari kama bidhaa na juic kwa wakulima wadogowadogo. miwa ni zao linalochukua muda mrefu kukomaa na kuvunwa kwa ajili ya kuuzwa kiwandani ili kutengeneza sukari. Kwa wakulima wadogo wanaweza kulima miwa kwa sababu ni zao lisilo na garama kubwa kwa uendeshaji na lina faida nzuri linapostawi vizuri na mavuno kuwa mengi ya kutosha.

  Miwa hulimwa sehemu zenye maji ya kutosha mvua za kutosha ili kupunguza garama za umwagiliaji, ukumbuke kuwa miwa huhitaji maji ya kutosha ili lkuweza kuzalisha tani za kutopsha pind unapovuna. ni vyema kufwata ushauri na utaalamu kwenye kilimo hiki ili kuweza kuzalisha kiasi kikubwa cha miwa na kupata sukari ya kutosha.

  KUANDAA SHAMBA
Shamba la kupanda miwa ni vyema liandaliwe mapema na kama ni jipya kabisa inatakiwa kusafishwa kabisa na kutlew visiki vyote ndipo uanze kulima, unatakiwa kulima mara mbili ndipo upitishe jembe la kusawazisha ili shamba liukae vizuri. Ikumbukwe kwamba kilimo cha mua kinataka aridhi iliyo laini na tifutifu ili kuupa urahisi mua kupeleka mizizi mbali kujitafutia chakula na kukua kwa urahisi.

   KUANDAA MBEGU
 Mbegu ya miwa inatakiwa kuandaliwa mapema sana kwa kumwagiliwa sana ili iwe laini vizuri na iweze kuchipua haraka pindi inapopandwa. Ni vyema mbegu ivunwe kwa wakati wa kupanda ili isije nyauka na kuykauka kabla ya kupanda. Mbegu ya uma inatakiwa kukatwa katika pingili ndogo ndogo tatu hadi nne kuiweka tayar kwa kupandwa

kwa leo tutaishia hapo tutaendelea kwa wakat mwingine na makala yetu ya kilimo cha miwa. TUNASHIDWA KUTUMA MAKALA MARAKWA MARA KULINGANA NA MAZINGIRA YA MASHAMBANI HUWA MTANDAO WA INTERNET UNASUMBUA KIDOGO ILA NATUJITAHDI WAPENDWA WANGU
    kwa ushauri na msaada wa mazao mengine wasiliana nai kwa
no0686060797

email;robinpraise5@gmail.com

Maoni 6 :

  1. Kutoka Mufindi Iringa Naaitwa ERICK PAULINUS MALATA Nimelifurahia somo katika makala yako nimejifunza jambo muhimu sana nililokuwa nalitamani siku nyingi,naomba kuuliza swali moja tu kama sio mawili je,inafaa kupanda miwa moja kwa moja bila kuiandaa kwenye kitalu? na je, kama sina mbolea ya samadi naweza kupandia DAP au MOP mojakwamoja yani natia mbolea na kuweka muwa? na je, inafaa kuacha miwa mingapi kwenye kila shina? AHSANTE SANA= malataerick@gmail.com/ 0768119595

    JibuFuta
  2. Tunaomba mwendelezo wa makala ya kilimo bora cha miwa

    JibuFuta
  3. Ahsante kwa somo lako,nahitaji kufahamu jambo moja muhimu,je yafaa kiasi gani cha fedha kiandaaliwe kwa ajili ya kuanza kilimo Cha miwa kwa hekari moja?

    JibuFuta
  4. Naomba kujua spacing za zao la miwa

    JibuFuta
  5. Nimefurahi sana kupata somo hili na natamani nije nianzishe mradi huu ila naomba kuuliza ulimaji wa miwa unaweza kugalimu kama sh. Ngapi na ni aina gani ya miwa inayotoa kiasi kikubwa cha sukari?

    JibuFuta