KILIMO CHA PAPAI
Jinsi ya kuandaa miche ya papai
karibu tena kwenye kilimo pendwa sana tanzania cha papai ambacho kinafaida ya kutosha sana
leo tutaangalia jinsi ya kuandaa miche ya papai tu.
Mbege za papai ni mbege ambazo zinachukua mda kidogo hadi kuchipua kwenye kitalu. hivyo zipo njia maalumu na bora za kufanya ili kuweza kuandaa mbegu zako. Nazo ni ;
-loweka mbegu zako na maji safi kwa muda wa siku tatu, huku ukibadilisha maji kila baada ya masaa 24 ai siku moja
-baada ya siku tati zitoe na uziweke kwenye kitambaa safi chenye matirio ya pamba
- funika vizuri ni uhakikishe hazipakiani kila moja iwe na nafasi yake
-kitambaa kiwe na unyevu na fukia kwa ondongo kidogo ili kuifanya iwe na joto iweze kupasuka haraka
-hakikisha kila siku jioni unamwagilia ile sehemu uliyofukia kitambaa chenye mbegu
- andaa viriba vyako tayari kabla mbegu hazijapasuka(kuchipua)
- mbegu zitachukua siku 5-8 kuanza kuchipua na unatakiwa kuanza kuhamisha zile zilizokua tayari zote
- pulizia dawa za kuua wadudu wa kwenye udongo kabla hujahamisha mbegu kutoka kwenye kitambaa
- zoezi hili lifanyike siku 2-3 kabla ya kupanda miche kwenye viriba
-tumia kitu chenye ncha kali il usijevunja mizizi wakati wa kupanda kwe viriba
fukia kidogo sana kwa mbaliii
-mwagilia vizuri kwa upole usijechimba mbegu na maji
mfano wa miche ya papai;
1;1 hiki ni kitalu cha papai siku mbili baada ya kuhamisha mbegiu hapo
1;2 hapo ni baada ya siku 5 baada ya kuhamisha mbegu za papai
karibun kwa ushauri na kufanyiwa kazi za usimamizi wa shamba. Tupo Kigamboni (kibada) Dar Es Salaam
MICHE YA PAPAI PIA INAPATIKANA KARIBUNI WOTE( TUNAFIKA KOTE TANZANIA)
imeandaliwa na
Mtaalamu wa kilimo
Robin Praise Kashanga
kwa mawasiliano
0686060797
email; robinpraise5@gmail.com
facebook; robin praise
insagam; agribusness-tanzania or robin-praise