Jumapili, 23 Septemba 2018

   Habarin za siku ndugu wasomaji wa blogg ya kilimo bora tanzania?  ni matumaini yangu kuwa ni wazima wa afya. Nimekuwa kimya kwa muda mrefu samahanini sana kwa kuwakosesha masomo muhimu yahusuyo kilimo na ufugaji yote hayo yalikua nje ya uwezo wangu. Karibuni tena tutakua pamoja kuanzia sasa tukijifunza mambo mengi kuhusu kilimo na ufugaji wa kisaa ili kujikwamua kiuchumi.
      leo napenda kuwapa somo zuri litakalowasaidia hasa wakulima wa mazao ya mboga mboga ndani na nje ya Tanzania.
    kilimo cha mboga mboga (BUSTANI) ni kilimo kizuri ambacho kina manufaa makubwa nadani ya familia na jamii zetu kwa ujumla. Kilimo cha bustani hakibagui ulime mboga gani kwa wakati unaofaa isipokua kwa anaelima kwa lengo la biashara lazima aangalie msimu na mahitaji ya soko ndipo alime kulingana na research aliyoifanya.
   kilimo cha bustani si cha kina mama au kina baba ni cha mtu yeyote aliye na nguvu na uwezo wa kulimaaa. Vijana wengi hawapend kufanya kilimo cha bustani kwa sababubu wanadhani hakiwezi kuwapatia kipato cha kuwatosha; mm nakanusha kwa kusema kilimo cha mboga mboga ni kizuri na kinafaidakubwa endapo utaamua kukilima kitaalamu.
    mara nying wakulima hulalamika kukosa mavuno mazuri na wakati mwingine kukata tamaa kabisa napenda kuwapa moyo kuwa ukiona mavuno yankua hafifu jaribu kutafuta wataalamu hata wa kujitegemea ili waweze kukushauri nn cha kufanya ili upate mavuno ya kutosha.
ANGALIZO;
   ni vyema kutafuta soko mapema ili unapolima uwe na uhakika wa kuuza mazao yako bila kupoata hasara. tumia mitandao ya kijamiii kutafuta masoko na wataalamu na si kushindia kuchart tu kama ilivyo kwa vijana wengi wa kisasa.
MBEGU;
    ni vyema kwa wakulioma wote kutumiaa mbegu za kisasa (hay breed) ili kuweza kupata mazao ya kutosha kulingana na mbegu yenyewe. Ni vyema kutumia mawakala waaminifu ili kuepuka kupewa mbegu zilizo pitwa na muda au kuchakachuliwa. kuna baadhi ya mawakala wasio waaminifu hasa maeneo ya vijijini hivyo unapo nunua mbegu jitahdi uwe mdadidisi ili usipewe mbegu isiyo bora kwakoooooo.
 MBOLEA;
   ni vyema kutumia samadi kwa wingi na mbolea za kisasa kiasi kwa ajili ya kupandia na kukuzia mmea ili uwe na afya nzuri na uwe na matunda ya kutosha na bora. Wakulima wengi hutumia mbolea kichoyo kwenye mimea na wakikosa mazao ya kutosha wanalalamika tumia mbolea kulingana na maelekezo kwenye kibandiko cha mbolea au kutoka kwa mtaalamu aliyekaribu yako.
HUDUMA KWA UJUMLA;
   Namaanisha umwagiliaji palizi vyote vinatakiwa vifanyike kjwa wakati ili kupata kitu kilicho bora yaani mazao mengi na bora kutoka shambaani kwako. Kuikagua mimea yako kila asubuh na jioni ili kubaini tatizo mapema kabla halijawa kubwa ili uweze kulitatua ipasavyo.
   
  Ndugu msomaji (MKULIMA) kilimo hakitaki presha wala harakaharaka unatakiwa ujipange na ujitoe kuwa mkulima kwelikwelii. Usiogope changamoto za kilimo bali kabiliana nazo maana hakuna kazi isiyo na changamoto katika ulimwengu huu.
  niombe ushirikiano wenu katika swala zima la kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa ili tujikwamue kiuchumi na kimaisha piaa.
   ukiwa na swali uliza ukiwa na maoni (coment) tumaa utasikilizwaa 

Imeandaliwa na afisaa kilimo
   Robin Praise Kashanga
  anaepatikana kwa
   namba 0768092549, 0625473643
   email; robinpraise5@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni