Alhamisi, 5 Machi 2020
KILIMO CHAAPAI SEHEMU YA PILI
Papai ni zao la biashara Kama tunavyo fahami pia hutumika kama lishe majumbanii kwetu
KUHAMISHA MICHE SHAMBANI
tunavyofahamu baada ya kuandaa Miche kwenye kitalu lazima tuihamishe shambani. Miche ya papai huhamishwa shambani pale inapokua na urefu wa sentimita 10 na kuendelea Hadi 30. Ni vyema Miche ihamishwe mapema ili kuipa uwezo mzuri wa kukua vizuri shambani.
KUANDAA MASHIMO
lazima shimo liandaliwee vizuri pana na refu ili kuipa uwezo mzuri papai kutanuka na kiweza kujitengenezea chakula Cha kutosha. Shimo la papai linatakiwa liandaliwee kwa kimo Cha upana wa sentimita 60 na urefu sentimita 60 piaa.
UWEKAJI WA MBOLEA
Lazima mbolea ya samadi itumike ya kutosha ili kiweza kuipa mche maisha marefu na kuhimili Hali ya udongo uliopo. Kila mche unatakiwa uwekwe plastiki moja ya mbolea ya samadi kabla ya kupanda mche, pia mwagilia maji ya kutosha kwa muda wa siku mbili ili mbolea ipoe ndo upande mche kwenye shimo lako
UMWAGILIAJI
lazima kuwe na kiwango maalumu Cha maji kumwagilia kwenye mche unaweza kuweka kiwango kulingana na Hali ya hewa ilivyo lakin Kama hakuna joto Sana kwa siku papai inatakiwa ipate maji Lita 5 kwa siku
PALIZI
Ni vyema kupalilia shamba lako kila wakati pale tu unapo ona magugu yameota. Ni vyema shamba Liwe Safi na pia ili mmea usipokonyane virutubisho na magugu shambani
KARIBU SANA KWA MUENDELEZO WA MAKALA HII YA KILIMO CHA PAPAI KIBIASHARA
Asante kwa kuwa pamoja nami
Afisa kilimo Robin praise
Sim 0686060797
robinpraise5@gmail.com
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)