Alhamisi, 10 Novemba 2016

KILIMO CHA MAHARAGE(Beanz)
    maharage ni zao ambalo hutumika kwa chakula na mboga pia kwa maisha ya mwanadamu. maharage ni chakula muhimu huongeza protein mwilini nakuufanya mwili kuwa na mguvu vizur. Maharage hutumiwa kama chakula kila siku kwenye mlo hivyo huhitajika kwa kiasi kikubwa

  KUANDAA SHAMBA
ni vyema shamba kuandaliwa kwa kutifuliwa vizuri kabla ya kupanda maharage. Shamba mbalo halitalimwa vizuri linaweza kusababisha ukosefu wa mazao kwa wingi. Unaweza kuandaa shamba kwa kutumia jembe la mkono trekta na plau pia.

     MBEGU
Maharage yapo ya aina mbalimbali ila tutazungumzia ani mbili ambazo ni bora na zenye uzao mwingi. aina moja wapo ni
   UYOLE     04
Hii ni mbegu ambayo hukua kwa haraka sana na pia hutambaa. Mbegu hii huzaa maharage yenye ukubwa wa wastani na pia zinahimili magonjwa sugu yanayoshambulia magonjwa maharage kwa sana mfano kutu ya maharage
   Mbegu hii hupandwa mwezi wa 3 kama mvua zikiwahi , nakama mvua zikichelewa hupandwa mwezi wa nne. mbegu hii huchukua siku 105 kukoma
   kilo 75-90 hupandwa kwa hecta moja ambyo ni sawa na miche 195000-205000 ndani ya hekta moja. ndani ya hekta moja tunapata tarn 1.5-1.9 za maharage kama utakua umezingatia amsharti yotee.
  mbegu hii hukua kwa mikoa ya nyanda zajuu kaskazini, Mbeya, Iringa, Songwe, Rukwa na mikoa yote ambayo 800-2000 mm kutoka usawa wabahari

  PALIZI
ni vyema kupalilia maharege wiki mbili baada tu ya kuota vizuri ili kuondoa magugu yanayo nyonya virutubisho kutoka kwenye udongo ambavyo ni vya mmea husika ndani ya shamba lako. ukichelewesha palizi utasababisha maharage kudhoofu na kutotoa maharage kwa wingi.

NB
    wakati wa maharage kutoa maua usije ukapalilia wala kuvuruga maharage utadondoshs maua hivyo kupunguza uzalishaji mzuri wa maharage.
     Asanten kwa ushirikiano wenu wapendwa wotee

Kwa mawasiliano   0768092549,  0715876743
    emeil;robinpraise5@gmail.com
  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni